KUMBUKUMBU YA MELI KUBWA ILIYOZAMA (MV BUKOBA) MEI 21 1996,FLAVIANA MATATA AMKUMBUKA MAMA YAKE

image_1
Tanzania leo tumewakumbuka ndugu zetu ambao walipoteza maisha kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni mama mzazi wa mwanamitindo Flaviana Matata pamoja na mtoto wa mjomba wake ambao walikua safarini.
Leo Flaviana Matata akiwa na Ambwene Yesaya ‘Ay’ na baadhi ya wasanii wengine wa Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa dini waliungana na Watanzania waliopata nafasi kuhudhuria ibada iliyofanyika kwenye makaburi yaliyopo eneo la Igoma Jijini Mwanza.
image_4
Baba mzazi wa flaviana pamoja na wadogo zake
image_12
 
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family