Aliyekua
Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia Nishati,Mhe. George
Simbachawene (wa tatu kushoto) akikabidhi majukumu ya ofisi kwa Naibu
Waziri Mpya wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa
Kitwanga katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye
Ofisi za Wizara ya Nishani na Madini,jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia
ni baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo.
Aliyekua
Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia nishati, Mhe. George
Simbachawene akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya
Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga.
Na Asteria Muhozya
Aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia nishati Mhe.
George Simbachawene amemkabidhi majukumu ya ofisi Naibu Waziri
Mpya wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga
ambaye atashughulikia Nishati.
Wakati akimkabidhi majukumu hayo, amemmtaka Naibu huyo kuhakikisha
anasimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini kwa kushirikiana na
Wakala wa umeme Vijijini (REA) ili kukamilisha ghughuli hiyo kwa wakati,
ikiwa ni pamoja na kukamilisha majukumu mengine ambayo ameyaacha
akiwa bado hajayakamilisha.
“Namwaachia ofisi yangu mtu mzoefu, na anayejua kazi kuliko mimi
naamini ataendeleza kile ambacho nimekiacha. Alisema Simbachawene.
Akizungumzia majukumu yake mapya katika Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya makazi , ameeleza kuwa, anaamini atatekeleza majukumu
yake vizuri kutokana na kuwa na elimu na ujuzi wa masuala ya Sheria ya
Ardhi na Utawala hivyo anaamini atayasimamia majukumu yake mapya
vizuri.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayesimamia
madini Mhe. Charles Kitwanga, ameishukuru Wizara kwa mapokezi
aliyoyapata Wizarani hapo ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa majukumu
yake mapya aliyopewa na hivyo, kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili
kukamilisha yale ambayo amekabidhiwa.
“Nilipoteuliwa nilistuka kidogo, lakini baada ya kushiriki kongamano la
viongozi wa dini lililo jadili masuala ya rasilimali hizi za gesi,mafuta na
madini na taarifa mlizonipatia kuhusu nini natakiwa kukisimamia sasa nipo
tayari kuanza kazi’’. Alisema Kitwanga.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim
Maswi, amemkaribisha Waziri huyo na kueleza kuwa, wanatarajia
ushirikiano mzuri kwa kuwa anaamini anao uzoefu na uwezo mzuri
utakaosaidia kukamilisha majukumu yake aliyokabidhiwa ambayo kwa kiasi
kikubwa yanagusa masuala ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa na
Watanzania.
