MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Ahmed Ollotu ‘Mzee
Chilo’ amewatolea uvivu wasanii wasiopenda kushirikiana na wenzao
katika matatizo na kuwaonya kuwa tabia hiyo si nzuri kwani ipo siku
itawaponza.
Akizungumza na mwandishi wa GPL hivi karibuni katika mahojiano
maalumu, Chilo aliyejizolea heshima na umaarufu mkubwa katika fani hiyo,
alikiri kuwa wasanii wengi wamekuwa wakijitenga na wenzao wakati wa
matatizo jambo ambalo linakera na kuumiza.
Msanii huyo alisema hakuna binadamu anayejua hatima ya maisha
yake hapa duniani, hivyo ni vyema kuishi katika mwenendo ulio mzuri,
kwani watu wote ni udongo na mavumbini watarejea.
