
Juan Mata na Mzee Mourinho
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose
Mourinhoamesmea kuwa ulikuwa ni 'uamuzi mgumu' kwake kumwachilia
mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uhispania Juan Mata
kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya England Manchester United.
Mata aliye na umri wa miaka, 25, ameandikisha
rekodi ya uhamisho katika klabu ya Man United kwa baada ya kuuzwa na
Chelsea kwa kititia kinono cha pauni milioni 37.1.
Akizungumza na BBC Mourinho amesema:
" Haya ni maamuzi ambaye mkufunzi anapaswa
kufanya, lakini kwangu ilikuwa vigumu. Ningependa kuendelea kumwona
katika kikosi changu bila shaka,"

Juan Mata na mkufunzi David Moyes wa Man United
Lakini kuwa katika hali hii kwa mchezaji ni vigumu. Anastahili kuachiwa
milango wazi katika Chelsea. Napenda kuwaona watu wakiwa na raha.
Nasikitika sikuweza kumfurahisha katika kikosi hiki - nasikitika sana
kwa hilo, lakini najenga kikosi changu nikizingatia mchezaji Oscar
ambaye anacheza katika nafasi ya 10," anasema mzee Mourinho.
