KAMATI YA MAADILI CCM YATAKIWA KUWASHUGHULIKIA WALIOTANGAZA NIA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Philiph Mangula
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umeshauri Kamati ya Maadili ya CCM kuwaonyesha mlango wa kutokea wote walioanza kampeni za kugombea urais, ubunge na nyingine kinyume cha maadili ya chama.
Umesema wagombea hao ambao umewaita wasio rasmi, wameonywa mara kadhaa na viongozi wa chama ikiwamo kupitia kwenye vyombo vya habari, lakini wameshindwa kujitambua na kujirekebisha.
UVCCM umedai wagombea hao wasio rasmi katika kampeni zao tayari wameanza kusababisha kutoweka kwa mshikamano ndani ya chama, kwani wamekuwa wakipita nchi nzima kushawishi kwa fedha na rushwa nyingine mbalimbali makundi ya jamii ili kuungwa mkono.
Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, Paul Makonda alisema Kamati ya Maadili ya CCM ina wajibu wa kutafsiri hasira ya wanaCCM dhidi ya kampeni hizo ambazo zinakijeli chama, uongozi wa nchi uliopo na kuleta nyufa
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family