BREAKING NEWS.....MAGARI MAWILI YAWAKA MOTO IRINGA WAKATI WANAFUNZI WAKIJIFUNZA KUUNGA NGAO

Wananchi Iringa  mjini  wakilitazama daladala
  lililowaka  moto wakati likiwa kwa mafundi 
kuunga likichomelewa leo eneo la uwanja wa  samora
Daladala  likiwaka  moto  huku kikosi cha 
zimamoto na uokoaji  wakizima moto huo
Gari la Zimamoto na uokoaji mjini Iringa
 likizima moto  uliokuwa ukiteketeza 
daladala eneo la Samora  leo
Hili ni basi  ambalo pia  limewaka upande wa mbe
Konda  wa daladala  hilo akiwa na kifaa cha 
kuzimia moto ambacho  kimenusurika katika moto  huo
Mmoja kati ya askari wa  Zima moto 
mjini Iringa akilitazama daladala  hilo
Hivi  ndivyo  moto huo  ulivyoteketeza daladala  hilo
Askari  wa kikosi  cha  Zimamoto na uokoaji
 mjini Iringa Bw  JOhn Zacharia akikagua 
kifaa cha  kuzimia moto ambacho hata  hivyo

 kilikutwa  kikiwa  kibovu na si msaada  kwao
Bw Filibert Mwihava  akizungumza na mtandao  huu
Huyu ni mmoja kati ya mafundi  wazoefu ambao
  walikuwa  wamewaachia  wanafunzi hao kazi
BASI mmoja lanusurika  kuwaka  moto na daladala moja  yateketea yote kwa moto  wakati  wanafunzi  wa masomo ya  kuunga vyuma katika gereji  bubu  eneo
 la uwanja  wa  Samora  mjini  Iringa  wakijifunza  kuunga ngao  ya  daladala  hiyo 
yenye  namba za  usajili T189 AWN .

Tukio  hilo  limetokea  leo majira ya 2.15 mchana wakati  vijana  wawili wanaojifunza  kuunga   wakiendelea na  mafunzo ya  kuunga  ngao ya  daladala  hilo.

Akizungumzia ajali  hiyo mmoja kati ya  wafanyakazi wa gereji  hiyo Filibert Mwihava alisema  kuwa chanzo  cha  daladala  hilo  
kuwaka  moto ni  vijana  wawili ambao 
  wanajifunza  ufundi  wa  kuunga  vyuma
 katika eneo hilo kufanya  kazi  hiyo  bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo.

Kwani  alisema  vijana hao  walikuwa  wakiunga ngao ya nyuma ya  daladala  hilo
 jirani na tenki la mafuta  na kutokana na  cheche  zilizokuwa  zikitoka 

 zilisababisha moto kuibuka kwa kasi . Hata  hivyo  alisema mbali ya  kuwa na
 kifaa cha kuzimia  moto  bado walishindwa  kukitumia  kifaa hicho  kutokana na 

kutokuwa na elimu ya  kutosha  ya kukitumia. Mwihava  alisema kutokana na moto  huo kushika daladala  hilo linalofanya  safari   zake kati ya  Tumaini na Zizi la Ng'ombe  mjini  
  Iringa hakuna mtu  aliyezulika  zaidi ya  basi 
 lenye namba za  usajili T 457 AMQ kutetekea  upande wa  mbele  kabla ya  kuokolewa .
Pia  alishukuru  kikosi cha  zimamoto  na uokoaji mjini Iringa ambao  walifika kwa  wakati na  kufanikiwa  kuzima moto  huo ambao 
 ungeweza  kusababisha  madhara  makubwa katika  eneo hilo ikiwa ni
 pamoja na ofisi  maduka  ya  watu  waliojenga
  kuzunguka uwanja  wa  Samora  kuteketea.Akithibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo kiongozi wa askari wa zimamoto  ambao  walifika  
eneo hilo John Zacharia  alisema  kuwa  kuw
a  chanzo cha moto  huo ni uzembe wa ofisi  hiyo. Kwani  alisema hata  kifaa cha zimamoto   walichokuwa  nacho kilikuwa hakifanyi   kazi kutokana na kuharibika muda mrefu.
Huku  kifaa cha  kuzimia  moto  kilichokuwemo katika daladala  hilo ni kifaa ambacho  kidogo  zaidi na maalum kwa gari dogo 
ambacho  pia  kilikuwa hakifanyi kazi Zacharia  aliwataka   wamiliki wa  vyombo
 vya usafiri  kuzingatia sheria  za  zimamoto  ya  kuwa na vifaa vya kuzimia  moto badala ya  
kudanganya na  kuona kama wanaonewa  pale
  wanapolazimishwa  kuwa na vifaa hivyo.
Kwa hisani ya Francis Godwin
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family