ALICHOSEMA BALOZI WA TANZANIA CHINA KUHUSU JACK CLIFF BINTI ANAYESEMAKANA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Jackie Cliff 13
Namnukuu Balozi ‘Ninazo taarifa nyingi ila ni kama mwezi uliopita alikamatwa Mwanaume, ni Wanaume waliokamatiwa Guangzhou,  mtu wangu aliekua anafatilia pia amekuja leo January 9 2014  asubuhi na kuniambia hakuna taarifa zozote kuhusu Jackline Patrick Cliff’

Kama ni Macao wangetuandikia moja kwa moja, Macao na Hongkong wangetuandikia moja kwa moja na kama wangekua wamewasiliana na balozi wetu wa heshima kule Hongkong pia wangetuandikia, Wachina mtu yeyote wanaemkamata ambae anatumia hati ya kusafiria ya Tanzania wanamuhusisha kama raia wa Tanzania kwa hiyo wanajulisha ubalozi wake labda mtu mwenyewe aseme ni wa taifa jingine, watatuandikia hivyohivyo nakueleza…..’
 Baada ya hayo maelezo ya Ubalozi wa Tanzania huko China, maswali yanabaki…. Jackie Cliff yukwapi? mbona marafiki wanasema hawampati kwenye simu? na huyu Mtanzania binti wa miaka 28 aliekamatwa Macao ni nani?
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family