Wengine 21 wajeruhiwa vibaya
Wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari ya Mustapha Sabodo iliyoko katika kijiji cha Msijute Halmashauri ya Mtwara Vijijini, mkoani Mtwara wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari wakati wakikimbia mchakamchaka jana alfajiri.
Wanafunzi hao walikufa baada ya kugongwa na gari aina ya Mercedes-benz namba T174 AED jirani na eneo la shule.(MM)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,
Zelothe Stephen, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea alfajiri saa
11:40 katika maeneo ya shule hiyo barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi na
kwamba gari hilo lililokuwa katika mwendo wa kasi, lilikuwa
linaendeshwa na Baraka Mgengwe (50) wakati likitokea Mtwara kwenda
Lindi.
Kamanda Stephen hakutoa maelezo zaidi
kuhusiana na mazingira ya ajali hiyo, mbali ya kusema kuwa wanafunzi hao
walipatwa na mkasa huo wakati wakigeuka kurejea shuleni.
Alisema kuwa wanafunzi 21 walijeruhiwa huku wengine 26 waliopata mshtuko, walitibiwa kisha kuruhusiwa.
Alisema dereva wa gari hilo anashikiliwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kamanda Stephen aliwataja wanafunzi waliokufa kuwa ni Khairath Mohammed, Mwanahamis Mohammed, Hasma Mpunja na Hilda Mathias.
Kamanda Stephen aliwataja wanafunzi waliokufa kuwa ni Khairath Mohammed, Mwanahamis Mohammed, Hasma Mpunja na Hilda Mathias.
Maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.
Alisema polisi walipata taarifa muda mfupi baada ya ajali hiyo na kufika eneo la tukio na kushiriki kuwapeleka majeruhi hospitali.
Alisema polisi walipata taarifa muda mfupi baada ya ajali hiyo na kufika eneo la tukio na kushiriki kuwapeleka majeruhi hospitali.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Vijijini,
Wilman Ndile, alisema uongozi wa wilaya yake umeunda kamati inayoongozwa
na mganga wa wilaya na ofisa elimu kushughulikia mipango ya kusafirisha
miili kwenda katika maeneo yao kwa ajili ya mazishi.
Mganga Mkuu wa Hospitali Rufaa ya Ligula, Dk. Shaibu Maarifa, alithibitisha kupokea majeruhi na maiti.
Mganga Mkuu wa Hospitali Rufaa ya Ligula, Dk. Shaibu Maarifa, alithibitisha kupokea majeruhi na maiti.
Dk. Maarifa alisema madaktari na
wauguzi wa hospitali hiyo walijipanga kuhakikisha wanaokoa maisha ya
majeruhi na kwamba wanaendelea vizuri, isipokuwa mwanafunzi mmoja wa
kike hali yake siyo nzuri.