![]() |
TIMU ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20
(Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa
ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza
Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa
Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida
Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia
Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred
utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) LEO Jumapili
(Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
|
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
8 months ago

