


Msanii Judith Wambura, Lady jay dee na Joseph Haule, Prof Jay wakishirikiana kuimba kibao cha joto hasira kwa maelfu ya mashabiki wa muziki waliojitokeza katika Tamasha la Burudani la P Square lililofanyika viwanja vya leaders club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akitoa burudani ya aina yake kwa maelfu ya Mashabiki waliojitokeza katika viwanja vya leaders club, Tamasha hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania burudani hiyo ya karne ilitolewa kwa mashabiki wa muziki pale leaders club.

Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akionesha uwezo wa kulimudu gitaa tofauti na kuimba tu, wakati wa tamasha la burudani lililofanyika katika viwanja vya leaders club, Wasanii hao mapacha walikonga nyoyo za maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Wanamuziki wa kundi la P Square, wakikonga nyoyo za mashabiki wa burudani waliojitokeza katika Tamasha la burudani lililofanyika katika viwanja vya leaders club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Wasanii hao walitoa burudani ya karne kwa mashabiki wa muziki nchini na kuacha historia ya kipekee kwa mashabiki wao kwa kufanya shoo ya masaa mawili mfululizo.


Msanii Judith Wambura, Lady jay dee akiteta jambo na wasanii wa musiki wa kundi la P-Square kabla hawajapanda jukwani na kutoa burudani kali kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo lililofanyika viwanja vya leaders club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania
Dar es Salaam, 24 Nov 2013 . . Siku ya jumamosi mwezi huu pale
leaders club ilikuwa Usiku ya kihistoria kwa tasnia ya burudani nchini
Tanzania baada ya wasanii mapacha wa kundi la P Square, Peter na Paul
Okoye kutoa burudani ya aina yake ambayo haijapata kutokea kwa muda
mrefu hapa nchini kwa maelfu ya mashabiki wa burudani waliojitokeza
katika viwanja vya leaders club.
Wakiwa ni wasanii wanaokonga nyoyo za mashabiki wa muzikini barani
Afrika walisindikizwa na wasanii kutoka hapa nchini ambapo jukwaa
lilifunguliwa na msanii Ben Pol ambaye alikonga nyoyo za mashabiki wa
muziki kwa kuimba kwa muziki wa bendi uliokuwa ukipigwa live na bendi ya
machozi bendi.
Huku hamu ya mashabiki wa burudani ikianza kukolea kazi iliyofanywa
vyema na mwanadada Rady Jay dee iliwatoa jasho mashabiki waliofurika
katika viwanja hivyo, huku akiimba wimbo wa joto hasira uliopokelewa
vyema na mashabiki ulimshuhudia Profesar Jay akipanda jukwaani huku
akichana sehemu ya wimbo huo alioshirikishwa na mwanadada Anaconda.
Kazi ya burudani kwa wasanii wa Tanzania ilifungwa vilivyo na msanii
Jo Makini au mwamba wa kaskazini alie limudu jukwaa na kuwapagawisha
vilivyo mashabiki wa muziki huku akisaidiwa vyema na msanii mwenzake
Niki wa Pili ambao kwa wasasa wanatamba na kibao chao cha tatizo ni bei
ya mkaa kilicho pokelewa vyema na mashabiki wao.
Ulifika wakati ambao ulitarajiwa na maelfu wa mashabiki waliojitokea
katika viwanja vya leaders club ambapo wasanii Peter na paul okoye,
walipopanda jukwaani na kuanza kutoa burudani kwa mashabiki. Wasanii hao
walianza kwa kuwashukuru mashabiki waliojitokeza na kuishukuru kampuni
ya Vodacom kwa kufanisha ujio wao hapa nchi.
P Squre walitoa burudani ya kipekee kwa muda wa masaa mawili
mfurulizo bila ya kuchoka na kila walipoweka kibao kingine ndipo moto wa
mashabiki ulizidi kuwaka na kukidhi vilivyo kiu ya mashabiki wa
burudani.
Burudani ya kipekee ilikuwa pale ambapo wasanii hao walianza kuonesha
vipaji tofauti walivyonavyo, huku Peter akionesha uwezo wa kupiga gitaa
vilivyo alijibiwa na kaka yake Paul akijibu mapigo kwa kupiga vilivyo
ngoma huku wakipokea shangwe kutoka kwa mashabiki wao.
Shukurani za kipekee kwa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyofanikisha
ujio wa wasanii hawa waliotoa burudani ya kipekee kwa Watanzania hakika
itakuwa ni historia ya aina yake kwa tasnia ya burudani na fundisho kwa
wasanii wa hapa nchini.
