PETER OKOYE WA P SQUARE AFUNGA NDOA YA KIMILA NA MCHUMBA WAKE WA MUDA MREFU

Peter Okoye Akimvisha Mke Wake Pete Muda Mfupi Baada Ya Ndoa Hiyo Ya Kitamaduni Kufungwa
Nyota Wa Muziki Afrika,Wanaofanya Kazi Kwa Kushirikiana..Wakiwa Wamezaliwa Mapacha Kutoka Katika Familia Ya Mzee Okoye Wenye Asili Ya Nigeria Hapa Nawazungumzia Peter And Paul Okoye,Waliokamata Soko La Mziki Wa Afrika Hata Duniani Pia Huku Nyimbo Zao Zikiendelea Kusumbua Kila Kukicha.Tarehe 17 Mwezi Huu Mmoja Kati Yao Ameuaga Usela Ambaye Ni Peter Baada Ya Kumuoa Mchumba Wake Wa Siku Nyingi Anayejulikana Kama  Lola Omotayo Kwa Ndoa Ya Kitamaduni Zaidi Iliyohusisha Nchi Yao.
Mastaa Wengi Wamemsindikiza Akiwepo Na Pacha Wake Ambaye Ni Paul Huku Wasanii Na Watu Maarufu Nchini Humo Na Hata Nje Ya Nchi Walihudhuria Ndoa Hiyo Akiwemo  Na Msanii Kutoka Tanzania  Anayefanya Vizuri Africa Na Ndani Ya Nchi Yake Pia Anaaminika Kua Msanii Namba Moja Anayeingiza Mkwanja Mrefu Zaidi Kuliko Wenzake"Nassib Abdul Jumaa"Maarufu Kama Diamond Platnumz Nae Amehudhuria Ndoa Ya Star Huyo Wa Nigeria Na Dunia Nzima Peter Okoye.

Zifuatazo Ni Picha Za Watu Mbalimbali Waliohudhuria Sherehe Hiyo
Muonekano Wa Ukumbi Kwa Mbele
Nembo Iliyoonekana Mbele Ya Ukumbi Huo Ikiwa Imebeba Herufi Za Bwana Harusi Peter Ikiwa Kama "P" Na "L" Ikiwa Imesimama Kama Jina La Bibi Harusi Anayefahamika Kama Lora

Diamond Akiwa Na Mdau Wa Muziki Nchini Humo(Kushoto) Kulia Ni Msanii Wa Muziki Nigeria "IYANYA"

Diamond Platnumz Kutoka Tanzania Akiwa Katika Pozi Na Bwana Harusi

Diamond Na Iyanya Katika Pozi


Paul Ambaye Ni Pacha Wa Bwana Harusi Peter Akiwa Katika Pozi Na Mwanae

Peter Na Mke Wake Muda Mfupi Baada Ya Kufunga Ndoa


Moja Ya Sehemu Katika Ndoa Inayohusisha Mila Zao Zikiendelea Ukumbini Humo

Peter Na Mkewe Wakikata Keki


Peter Akiwa Na Mchezaji Maarufu Wa Soka Adebayor







Genevieve Muigizaji Wa Filamu Nchini Nigeria Nae Alikuepo

Peter Na Mkewe Wakicheza Kwa Furaha

Peter Na Mkewe Katika Tabasamu



Peter Na Wapambe Wake Ukumbini

Katikati Ni Mke Wa Peter Akiwa Na Marafiki Zake

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family