skip to main |
skip to sidebar
MSANII WA KWANZA TANZANIA AMBAYE MH BARACK OBAMA AMEMFOLLOW KATIKA MTANDAO WA TWITTER
Hii
itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika
kuwa followed na Rais Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana
zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita.
Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais
Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu
kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya
ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow.
Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.


