Familia iliyohusika kumsaka kikongwe Helena Petri siku aliyopotea.Picha na Juma Mtanda
Na Juma Mtanda, Mwananchi
Mwenyekiti huyo wa Kitongoji cha Gongo, Festo
Mfaume katika mahojiano na mwandishi wa makala haya anasema,“Kitongoji
changu kina zaidi ya wananchi 325 na tukio hili la kuchunwa ngozi mtu
limekuwa la kwanza kutokea. Nilichofanya ni kuwatawanya watu katika
makundi kuingia kwenye misitu na vichaka.
Morogoro. Tukio la kifo cha
kikongwe, Hellan Petri Mahunzila (75) ambaye alipotea katika mazingira
ya kutatanisha kwa siku 12 kisha siku ya 13 mwili wake kuonekana kando
ya shamba lake huku mwili wake ukiwa imechunwa ngozi mwili mzima,
imezua hofu kubwa.
Wakazi Kitongoji cha Gongo, Kijiji cha Mgata, Kata ya Bwakilajuu mkoani Morogoro, ambako tukio hilo limetokea, sasa wanaishi kwa hofu.
Baadhi yao wanalazimika kujisaidia haja ndogo na kubwa katika makopo hasa nyakati za usiku, ndani ya nyumba zao. Tukio hilo limebadili kabisa mfumo wa maisha na kutembea, wengi wanalazimika kuingia ndani ya nyumba kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12:30 jioni wakihofia kutekwa.
Tukio lenyeweNi saa 7 usiku, siku ya Jumatano kuamkia Alhamisi ya Oktoba 2 mwaka huu, Eliza Steven (19) anaamka na kumnyonyesha kichanga chake, James Peter (miezi mitatu), baada ya kilio cha mtoto huyo mchanga kuhitaji kunyonya.
Baada ya James kunyonya na kushiba, alinyamaza kulia, hiyo ilikuwa ni kama kumpa fursa mama yake kutoka ndani ili aende nje kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo.
Anafungua mlango wa chumba chake na kutoka nje kujisaidia huku akipiga jicho na kuangalia mlango wa chumba anacholala bibi yake, anaona mlango upo wazi. Jambo hilo, hakulitilia shaka sana kwani alikuwa na imani angeweza kukutana naye nje ama chooni, haikuwa hivyo.
Alilazimika baadaye kuingia chumba anacholala bibi huyo, aliangalia kitandani ili kuweza kujibu maswali yake yaliyojaa kichwani likiwamo la kwa nini bibi yake ameshindwa kufunga mlango kama alitoka nje? Anaanza kusema Eliza. Eliza aliendelea kueleza kuwa baada ya kuchunguza katika chumba kile kinachotumiwa na bibi yake, Hellen ambaye alikuwa na kawaida ya kufunga mlango pindi aiingiapo kulala, hakumwona na kuchukua jukumu la kumwamsha mama yake mzazi, Yustina Kasian (40) ili aweze kusaidiana naye kumtafuta.
Yustina Kasian ambaye ni mtoto wa pili kwa kuzaliwa kwa bibi, Hellen Petri Mahunzila anasema baada ya kuelezwa maneno yale na mtoto wake, Eliza Steven ambaye ni bibi yake alienda katika kile chumba anacholala mama yake na kuangalia huku na huku, bila mafanikio.
“Nilienda chooni na kuangalia ndani ya choo lakini sikumwona, nilirudi ndani na kumwamsha mume wangu, Steven Francis (50) ili naye atusaidie kumfuata kwani tayari hofu ilianza kutanda moyoni mwetu na kujiuliza maswali ambayo hatukuweza kupata majibu usiku ule,” anasema Yustina.
Mimi baada ya kuelezwa jambo hilo na mke wangu nilitoka nje na tochi hadi chooni na kumulika ndani na kuzunguka kile choo, sikuweza kumwona. Nilienda pia kumtafuta kwenye banda la kupikia na eneo zima la migomba lakini mama mkwe wangu hakuweza kuonekana akiwa hai ama amekufa,” anasema Steven Francis.
Francis anasema baada ya kushindwa walikwenda kwa majirani kuomba msaada wa kumtafuta; walikwenda kwa jirani Selis Silili na Calist Stephano.