![]() |
Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa
wa Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu
aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.
Baba mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi 87.5 Shinyanga amesema
‘kwenye mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya
baada ya kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi
ila watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika
na tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa
mirathi’
‘Watoto walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa
shemeji yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo
yani haya majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama
Kanumba ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana
nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo
aisee patachimbika’ – Baba Kanumba
Kwenye sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke
wala mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili
mimi na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na
Mama Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’
Baba Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana
na kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa
kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua
nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.
|
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
8 months ago

