![]() |
| Aliyewaua Wenzake |
Mfanyabiashara
wa jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina la Gabriel Munisi amefanya
mauaji kwa watu wawili na kujeruhi mmoja kisha kujiua kwa kujipiga
risasi katika tukio lililotokea leo asubuhi eneo la Ilala Bungoni jirani
na Klabu ya Wazee jijini Dar es salaam.
Tukio
hilo lililo husishwa na wivu wa mapenzi limetajwa kufanywa na Munisi
baada ya kuabini nyendo za kusalitiwa na mpenzi wake aliyetajwa kwa jina
la Christina Nando.
![]() |
| Aliyeuwawa Ndani Ya Gari |
![]() |
| Damu zikiwa zimetapakaa eneo la tukio .
Akiwa
kwenye gari lake Munisi aliwafyatulia risasi marehemu waliokuwa
wakitoka getini wakiwa kwenye gari lao hivyo kumpiga risasi dereva wa
gari hilo, Francis Samwel, Christina Nando na watu wengine wawili
waliokuwapo ndani ya gari hilo ambapo mmoja ni mama mzazi wa Christina.
Kwa
mujibu wa taarifa za awali zinasema watu wawili walifariki dunia papo
hapo kutokana na tukio hilo na wengine wawili kujeruhiwa.
|
![]() | |
| Gari Lililoshambuliwa Katika Tukio Hilo
TAARIFA ZAIDI
Mapema
leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala
Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu
wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa
limetokana na wivu wa kimapenzi.
Dereva
mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza,
alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu,
ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye
alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu
nyingine.
Kwa
mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka
aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo
MM.
Mara
baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila
cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa
anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.
Wakati
jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf
ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa
akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.
|
![]() |
Jamaa
akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari
hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja
la Carol, hii ni kwa mujibu wa dereva huyo na mara baada ya kuona hivyo
hivyo ikabidi akimbie.
Vyanzo
vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya
mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine
risasi ya mguu.
Mtuhumiwa
na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana
mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
Bado
haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo licha ya watu wengi
ambao nilipata bahati ya kuongea nao wakilihusisha tukio hilo na mambo
ya kimapenzi.





