![]() |
| Katibu Wa Kamaati Ya Uhuru Marathon Bw. Innocent Melleck |
FOMU za
mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinatarajiwa kuanza
kuuzwa rasmi kuanzia kesho, huku Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa
kuchukua fomu namba moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya
Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, Rais Kikwete ndiye atakayepewa
fomu nambo moja kwa ajili ya kushirikishi mbio hizo.
“Hizi
mbio zina maana kubwa mno ndani ya Taifa letu, Rais Jakaya Kikwete muda
wote anasisitiza na kupigania amani. Amani ni yetu sote, si vyema
kumuachia Rais Kikwete peke yake kuipigania, hivyo yeye ndiye
atakayekuwa namba moja katika kuchukua fomu na kushiriki mbio hizo,”
alisema.
Melleck
alisema, katika kuhakikisha kila mtu anashiriki kutakuwa na vituo 13
vitakavyofunguliwa kwa ajili ya kutoa fomu hizo, huku pia kukiwa na watu
maalumu watakaozisambaza maofisini na hata majumbani.
Melleck
alisema, fomu hizo zitatolewa kwa Sh 100,000 kwa wale watakaotaka
kukimbia mbio za kilomita tatu, Sh 2,000 mbio za kilomita tano, Sh 6,000
kwa atakayeshiriki moja kati yam bio za kilomita 21 au 42.
“Hizi
mbio ni muhimu zaidi kwa ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa
Watanzania wote wakashiriki ili kuipigania amani iliyopo nchini mwetu.
“Tunataka
kuungana na Rais Kikwete katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuleta
umoja, amani na mshikamano ndani ya Tanzania na ndilo lengu la mbio
hizi. “Bado
tunaendelea kuwaomba wadhamini wajitokeze kuzidhamini, kwani nafasi
bado ipo wazi na watambue hata wao ni sehemu ya kupigania amani ya taifa
letu,” alisema Melleck.
Katika
mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia
mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na
Full Marathon yenyewe kilomita 42.
Mratibu
huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi
wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia
zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
“Hapa
tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile
viongozi maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili
kushiriki, kwa kudumisha amani na upendo.
“Pia
tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia
watu wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa
wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,” Alisema.
Melleck alisema, wamejipanga mno ili kuhakikisha wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.

