Aidha CCM inamtumia salam za pongezi za
dhati Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba
27, 2013 jijini Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi, kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza
jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu
mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape
Nnauye anawaasa“Tunauomba uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi
na badala yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika
mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi”
“Daima
imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa
pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka"
Ndugu Nape amehitimisha.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro
imekuwa kwa sehemu kubwa chanzo cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa
nchini na hivyo kuwanyima Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye
mchezo huo na hasa pale timu zao zinapopata ushindi.
Imetolewa na:-
Kitengo
cha Mawasiliano na Umma
Chama
Cha Mapinduzi
Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu
Dar
es Salaam
|