BALOZI SEPETU ( BABA MZAZI WA WEMA ) KUZIKWA JUMATANO

Mwili wa Baba mzazi wa Wema Sepetu, balozi Isaac Sepetu ambaye alifariki siku ya jumapili asubuhi unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumatano asubuhi kuelekea Zanzibar ambapo shughuli za mazishi zitafanyika siku hiyo hiyo ya jumatano kisiwani huko.

Kupitia kipindi cha Kurasa cha EATV mtoto wa kiume wa Mzee Isaac ametoa ratiba kamili ya shughuli za mazishi zitakavyofanyika.
2brothers9093 Blog  inapenda kutoa pole kwa Wema Sepetu na familia nzima kwa msiba mzito uliowakuta. Tupo pamoja kwenye wakati huu mgumu.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI…!!
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family