BABY MADAHA AZINDUA MIFUKO YAKE YA KUBEBEA ZAWADI

Siku ya Ijumaa tarehe 25/10/2013 historia nyingine iliandikwa na queen of swaggz from Tzee Baby Madaha baada ya kuitambulisha rasmi bags zenye picha yake zinazotumika kubebea zawadi.
Katika party hiyo fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mziki wa bongo fleva na waandishi wa habari wa media tofauti tofauti ilifanyika kwenye eneo tulivu la hotel ya Den France iliyopo pande za Sinza kuanzia saa 2 usiku ikiambatana na bata la kufa mtu.

Baby Madaha anatarajia kutambulisha Perfume zenye sura yake akiwa chini ya lebo inayofanya poa pande za Kenya ijulikanayo kama Candy n’ Candy chini ya mkubwa Joe. In short mengi mazuri yanakuja kutoka kwa Baby Madaha na soon anaachia rasmi video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina la Mr. DJ iliyo kwenye mahadhi ya Dancehall.
Mdau Akionesha Moja Ya Mifuko Hiyo Ya Kubebea Zawadi Iliyozinduliwa Siku Hiyo

Baadhi Ya Wadau Waliohudhuria Uzinduzi Wa Mifuko Ya Kubebea Zawadi


 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family