PIGO BONGO MOVIE:MSANII WA FILAMU NCHINI JAJI KHAMIS ALMAARUFU KAMA KASHI AFARIKI DUNIA

Habari iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee masinde,samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.
Taarifa za awali zinasema kuwa alikuwa amelazwa hapo kwa muda kiasi kabla ya kufikwa na mauti hayo. Tutaendelea kuwajulisha zaidi punde tutakapoendelea kupata taarifa zaidi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameni

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family