Mazishi ya mwigizaji mwigizaji Jaji Khamisi (Kashi)
aliyefariki jana mchana kwenye hospitali ya muhimbili jijini Dar es
Salaam yamefanyika leo mchana majira ya saa nane kwenye makaburi ya
kinondoni jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikubwa na umauti baada ya kuugua ghafla malaria na kifua vilivyosababisha kufikwa na mauti hayo.
Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na waigizaji wengi wa tasnia
ya bongo movies yalitawaliwa na huzuni ikizingatiwa kuwa mwanadada Kashi
alikuwa ni mtu asiye na tatizo lolote na mtu na ni mtu aliyekuwa mpole
na mwenye upendo na watu wote.
Kabla ya kufariki marehemu alikuwa akiishi maeneo ya Kinondoni
Mkwajuni na mume wake na ndipo msiba wake ulipokuwa kwa siku hizi
mbili.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.

