KESI YA MH SUGU YAFUTWA

Picture
Mbilinyi akiingia mahakamani akiongozana na Mwanasheria wake, Lissu (picha: Lukwangule Ent. blog)
MWENDESHA Mashitaka wa Serikali (DPP) leo asubui aliambulia patupu baada ya Hakimu wa Mahamaka ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Dodoma, kumwachia huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, (CHADEMA) ambaye alimfikisha kizimbani kujibu tuhuma za kumkashifu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia mitandao ya jamii (bofya hapa kurejea kilichoandikwa).

Awali, Wakili wa Mbilinyi ambaye ni Mwanasheria na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Mb, CHADEMA), aliitaka mahakama ifutilie mbali shitaka alilofunguliwa mteja wake kwa kudai kuwa halina msingi wowote wa kisheria.

Baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na Mwanasheria wa Serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno, “mpumbavu” ni lugha ya matusi, ndipo Hakimu alipoamua kulifuta shitaka lililowasilishwa kwake na kumwambia DPP akatengeneze upya mashitaka yake kwani aliyoyapeleka yalikuwa na hitilafu kubwa.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family