![]() |
| Mwili wa marehemu Pepetua ukiwa unaingizwa kwenye gari la polisi mara baada yakuokotwa akiwa amechinjwa na kutupwa jalalani |
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanane, akiwamo
mfanyakazi wa ndani anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi mwenzake ajulikane
kama Pepetua Maina kwa kumchinja na kisha kuutupa mwili wake kwenye
shimo la taka.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana.
Alisema
Philemon Laiza (27), mkazi wa Mikocheni B, anatuhumiwa kuhusika na
mauaji ya Perptua Maina (30) kwa kumchinja na kisha kutelekeza mwili
wake kwenye dampo la takataka.
Kova alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Katika tukio
la pili, alisema watu wawili; Isaya Mafuru (31) na Yusufu Machela (33),
wanatuhumiwa kwa uporaji wa mali za raia wa Sweden, Gisela Bergstorm
katika maeneo ya Coco Beach.
Katika tukio
la lingine, alisema watu wanne, ambao ni Thenase Benjijimana (26), raia
wa Burundi, Said Hassan (37), mkazi wa Mbande, Obadia Bukuku (25) na
Benedict Mohamed (32) wakazi wa Tabata, wanatuhumiwa kwa kukutwa na gari
ya wizi aina ya Noah T 157 BWC, pamoja na pikipiki aina ya Boxer T 568
CDL.
Wote kwa pamoja wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Chanzo: Nipashe

