RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA

Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika
 katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert
 Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumapili kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini,
ukitokea nchini Afrika ya kusini.

 Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali
 ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni
 kwa hisani ya Clouds
Media Group. Ndio waliogharimia safari ya
mwili wa marehemu.

Baada ya Hapo, mwili wa Albert
 Mangwea utakuwa unaagwa viwanja vya leaders
club siku Ya Jumatatu na kampuni
itakayoshughulikia
zoezi hili ni Entertainment Masters na baada
 ya mwili kuagwa,
safari ya kumsindikiza Albert Mangwea
kuelekea kwenye maziko
 itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.




Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la
 Kihonda, mkoani,
Morogoro...!!

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family