POLISI NCHINI TANZANIA INAWASHIKIRIA WATU NANE WAKIWEMO RAIA WA SAUDI ARABIA KWA UHUSIKA WA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI ARUSHA

Polisi nchini Tanzania inawashikilia watu wanane kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa
siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi
Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.Wakati mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akuzungumza akiwa hospitalini mjini Arusha
amesema idadi ya watu waliofari dunia kufuatia mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama
ilivyoripotiwa hapo awali.Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi
ni wawili.Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni bomu aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.Lakini Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la tukio mbali na majeruhi hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia sakafi na kuta za kanisa hilo hazikuchimbika sana.Kutoka Dar es Salaam Leornad Mubali anaongezea kuwa watu wawili sana wamethibitishwa kufariki dunia katika mlipuko huo uliotokea majira ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mjiwa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa
kujeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya
uzinduzi wa parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia .Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye
ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo unapotokea walikuwa
tayari katika hatua ya kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa kanisa ulikuwa ukiongozwa na
balozi wa Papa Fransis.Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC
kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali watu kati yao
wamefariki huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha.Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo zimesitishwa huku watalaalamu wa milipuko na polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na
mlipuko huo.Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo ama kundi lolote
linalodaiwa kuhusika na utegaji wa bomu hilo.Hili ni shambulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japo kuwa mwaka huu pia kulikuwa
na mtukio ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family