Kiungo
wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima, akizungumza na Waandishi wa Habari
katika Makao Makuu ya Klabu ya timu hiyo, iliyopo mitaa ya Jangwani
wakati akitangazwa rasmi kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuitumikia
Klabu hiyo leo mchana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb.
**********************************************
BAADA
ya kumalizika kwa Filam ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kuanza kwa
Filam mpya ya Usajili, huku yakitawala maneno ya hapa na pale kuhusu
usajili wa wachezaji na na hasa mchezaji Haruna Niyonzima aliyekuwa
akielezwa kuwa alikuwa akiwaniwa na Mahasimu wakuu wa Yanga, Simba, na
huku ikielezwa kuwa 'eti' Mchezaji huyo alikuwa tayari ameshafanya
mazungumzo na Klabu hiyo kwa kumuongeza dau.
Klabu
ya Yanga Leo imeweka wazi na kumtangaza rasmi Niyonzima kuwa ni
mchezaji wao halali kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kwa
kumsainisha mchezaji huyo akiwa ni wa pili baada ya juzi tu kumrejesha
na kumsainisha mchezaji Mrisho Ngassa, aliyerejea nyumbani akitokea kwa
mahasimu wao Simba.
Hatimaye
kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili
Niyonzima, baada ya kusaini mkataba huo, amesema kuwa yeye ni mchezaji
halali wa Yanga na kwamba kesho anaondoka nchini kuelekea nchini kwao
Rwanda kwa mapumziko huku akijiandaa kwa ajili ya kuanza michuano ya
kutetea Kombe la Kagame.
Hata
hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la
Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga
imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.