Kamanda Sabasi aliwataja majina ya watuhumiwa tisa kuwa ni Victor
Ambrose Kalisti (20) mkazi wa kwa Mrombo Arusha na mwendesha boda boda,
Joseph Yusuph Lomayani (18) mwendesha boda boda na mkazi wa kwa Mrombo
Arusha.
Wengine ni George Bathoromeo Silayo (23) mfanyabishara na mkazi wa
Olasiti, Mohamed Sulemani Said (38) mkazi wa Ilala Dar Es Salaam na
huyu ndiyo mwenyeji wao aliyewafuata kwa gari binafsi uwanja wa ndege
Dar Es Salaam na kuwachukua hadi Arusha Hoteli ya Aquline.
Wengine wametajwa kuwa ni Said Abdallah Said (28, ambaye raia wa falme
za kiarabu, eneo la Abudhabi, Abdulaziz Mubarak (30) mkazi wa falmae za
kiarabu, eneo la Saudi Arabia, Jassini Mbarak (29) mkazi wa Bondeni
Arusha, Foud Saleem Ahmed (28) raia wa falme za kiarabu na Said Mohsen,
mkazi wa Najran falme za kiarabu.
Alisema kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea na mahojiano na tayari
jalada la mashtaka yao limepelekwa kwa mwanasheria Mkuu wa serikali, kwa
ajili ya maamuzi ya kisheria.
Kamanda Sabas alisema katika mahojiano na waandishi wa habari, alisema
kuwa katika hatua za awali zinaonyesha bomu hilo siyo la kienyeji na pia
wageni hao walikuw ana VISA halali ya kukaa nchini, kwa madai walikuja
harusini.
Alisema Watuhumiwa hao kutoka falme za kiarabu baada ya kuwahoji walidai wamekuja harusini.
Aidha alisema ulinzi umeimarishwa katika kanisa lilikotokea mlipuko la
mtakatifu Jospeh Mfanyakazi, Olasiti, ili kuhakikisha hakitokei kitu
chochote kabla na baada ya mazishi hayo