MBEYA:TCRA:SIMU ZISIZOSAJILIWA MWISHO JUNE MOSI

Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana. Mbeya Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu. Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali. Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana. Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku. Alisema kuwa ni muda mrefu umepita ambao ulitolewa kwa ajili ya kusajili namba za simu lakini watu wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa wakati na badala yake wamekuwa wakitumia simu vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya uhalifu na kutoa lugha chafu. Katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ilisema vyombo vya mawasiliano vimesaidia kukua kwa sekta mbalimbali .
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family