KILI MARATHON:MWANARIADHA KUTOKA TANZANIA AWATOA KIMASOMASO WATANZANIA AONGOZA MBIO ZA HALF MARATHON

KILI MARATHONI KENYA YATISHA - TANZANIA YAJIKONGOJA

MWANARIADHA wa Tanzania Sara Makela,amewatoa kimasomaso Watanzania baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za Half Marathon
kwa Wanawake,huku Wakenya wakiendelea kutamba katika mbio hizo zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini hapa.
Kwa matokeo hayo Sara,amejizolea Sh milioni 3.
Sara aliwashinda wenzake baada ya kutumia saa 1:13.05,huku akifuatiwa na Victoty Chepkemoni (Kenya), 1:14.34,Failuna
Malanga (Tanzania) 1:15.35,Joyce Kiplimoo (Kenya) , Paulina Muchiri (Kenya), Catherine Tuku (Tanzania), Nancy Kotich (Kenya),Jacinta Mboani (Kenya),Florence Cheruiyot (Kenya)
na Phylas Jelagat (Kenya).
Kwa upande wa Half Marathon Wanaume, Sila Limo (Kenya),aliibuka mshindikwa kutumia saa 1:03.46,hukumshindi wa pili akiwa Benard Kiprotich (Kenya), akitumia 1:04.00, wakatimshindi watatu ni
Charles Ogahri (Kenya),akitumia 1:04.25, Dickson Marwa(Tanzania), saa 1:04.30, Peter Kosgei (Kenya), akitumia saa 1:04.42, Evans Taiget (Kenya), akitumia saa 1:04.46,
Stephano Huche (Tanzania), akitumia saa 1:04.52, Patric Wambugu (Kenya),alitumia saa 1:04.56,Said Makula (Tanzania), akitumia saa1:05.03 na nafasi ya kumi ilishikwa na Peter Jule (Tanzania), aliyetumia saa 1:05.09.

Kwa upande wa Full Marathon kwa Wanaume, mshindi wa kwanza ni Kipsang Kipkemoi (Kenya), aliyetumia saa 2:14.56 na kujinyakulia Sh milioni 3, huku mshindi wa pili akiwa
Julius Kilimo (Kenya), akitumia saa 2:15.44 na kujinyakulia Sh 1.5, huku mshindi wa tatu akiwa Dominic Kangor (Kenya), akitumia saa 2:16.25 na kujinyakulia Sh laki
nane na nusu, nafasi ya nne ilikwenda kwa Onesmo Maitinya (Kenya), akitumia saa 2:16.36 na kujipatia Sh laki sita na nusu, huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Lioshiye Moikan (Tanzania),
akitumia saa 2:17.50 na kujipatia Sh laki tano, huku nafasi ya sita ikienda kwa Abraham Kipkosgei (Kenya),
aliyetumia saa 2:18.7 na kujinyakulia Sh laki 3 na nusu, nafasi ya saba ilishikwa na Alex Bartilol (Kenya), aliyetumia saa 2:18.14 na kujipatia Sh mbili na nusu,
wakati Justus Mebur (Kenya) alishika nafasi ya nane alitumia saa 2:18.16 na kujipatia sh laki mbili, wakati nafasi ya tisa ilishikwa na Eric Christopher (Kenya), aliyejipatia Sh laki moja
na nusu huku nafasi ya kumi ikienda kwa Antony Mugo (Kenya),aliyetumia saa 2:18.29.
Kwa upande wa Full Marathon Wanaume, mshindi alikua Edna Joseph (Kenya), aliyetumia saa 2:39.5, huku mshindi wa pili akiwa Eunice Muchiri, aliyetumia saa 2:41.00, wakati nafasi ya
tatu ilishikwa na Fridah Too (Kenya), aliyetumia saa 2:44.04, huku nafasi ya nne ilishikwa na Rosnline Daud (Kenya), aliyetumia saa 2:45.01, huku nafasi ya tano ikienda kwa Jane Kangora (Kenya), aliyetumia
saa 2:46.06, huku nafasi ya sita ikienda kwa Gladus Otero (Kenya), aliyetumia saa2:47.54, huku nafasi ya saba ikichukuliwa na Lilian Cheplimo (Kenya), aliyetumia saa 2:49.09, wakati nafasi ya
nane ilikwenda kwa Rosina Kibona (Kenya), aliyetumia saa 2:49.25, huku Seoflesina Sumawe (Tanzania0, akishika nafasi ya tisa kwa kutumia saa 2:50.11 na Eunice Korir (Kenya), akishika nafsi ya kumi kwa kutumia saa 2:52.21.
Hata hivyo wanariadha hao, watapatiwa zawadi zao baada ya kupimwa, mkojo ili kujirithisha kama hawajatumia dawa za kuongeza nguvu.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara, alisema riadha ni mojawapo ya michezo
inayoheshimika sana duniani.
"Niwakumbushe kuwa, mataifa ya Kiafrika ndiyo yamekuwa kinara wa kuzalisha wanariadha mashuhuri, nawaasa viongozi wa riadha Tanzania,
kuandaa mikakati shirikishi ya kukuza riadha na kuitekeleza ili nchi yetu iendelee kung’ara katika anga za kimataifa, kwa upande wa
wanariadha, nawasihi muendelee kujituma kwa kuwasikiliza makocha na viongozi wenu ili muweze kufanikiwa kuwa na viwango vitakavyowawezesha
kuwa na ushindani wa Kimataifa," alisema.
Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo
ni pamoja na Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel,
TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).














 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family