ADAN RAGE ANG`OKA SIMBA

WANACHAMA wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo wamefanikiwa kufanya mkutano wao ambao umeung'oa uongozi uliokuwa chini ya Mwenyekiti wake Aden Ismail Rage.
Mkutano huo licha ya kutokuwa na baraka ya uongozi wa sasa wa Simba, umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Star Light iliyopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanachama takribani 506 walihudhuria mkutano huo ambao umemalizika kwa wanachama hao kukubaliana kuuondoa madarakani uongozi wa Rage ambapo sasa klabu hiyo itaongozwa na Zacharia Hans Pope pamoja na Rahma Al Kharusi 'Malkia wa Nyuki' waliochaguliwa kama viongozi wa muda mpaka hapo watakapopatikana viongozi wapya.

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family