MWAMALALA AACHANA NA CHADEMA


EDDO MAKATA MWAMALALA
Na Gordon Kalulunga, Mbeya

MWANASHERIA Eddo Makata Mwamalala, ametangaza rasmi kuachana na chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuwa amechoshwa na kuchonganishwa na jamii na kutakiwa kuandika barua ya kuomba kugombea Ubunge 2015 makao makuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Mbeya Peack Jijini Mbeya leo, Mwamalala ambaye alikuwa katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya na Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa, alisema kuwa hivi karibuni kuna viongozi wamejitosa kumshambulia baada ya yeye kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kumtaka katibu mkuu wa chgama hicho taifa kujiuzulu baada ya kukiri kumiliki kadi ya CCM.

‘’Leo tarehe 03/01/2012 ni siku muhimu yenye kumbukumbu nyingi juu ya  maisha  yangu kisiasa. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kipengele cha 5.4 kukoma kwa Uanachama,  kifungu kidogo cha 5.4.1; nanukuu “ kwa kujiuzulu mwenyewe  kwa hiari yake.” Mimi Edo Makata Mwamalala leo hii naamua kutekeleza katiba hiyo; najiuzulu uanachama’’ alisema Mwamalala.

Alizitaja baadhi ya sababu za kuachana na chama hicho kuwa ni pamoja na kutokubaliana na Dr. Slaa kuwa na kadi ya CCM, matumizi ya Ruzuku si sahihi, huku Maafisa wa makao Makuu wakiishi kama wafalme na Malkia na kuwafanya wanachama wa Mikoani kama kuku wa kienyeji kwa kuwarushia  punje za mchele unapotaka kuwachinja.

‘’Mikoani viongzi na wanachama wanatoa pesa zao kwa kujichangisha kwa imani kuwa  siku moja watakula keki ya Ruzuku na ufadhili. Mimi nawahakikishia , kwa unyenyekevu  nilioufanya hawatopata hadi  Mbowe na Slaa watoke kwenye nafasi walizo nazo kwa sasa,wasidanganywe na siasa za mikutano ya matumaini ya kitaifa yenye posho’’ alisema Mwamalala.
Mbali na sababu hizo alitanabaisha kuwa sababu nyingine ya kuachana na Chadema ni mchakato wa mgombea  uraisi (2010) ndugu Slaa  kamati kuu ilipendekeza jina lake na kuitisha Baraza   kuu bila kuwasikiliza viongozi wenmgine wa mkutano mkuu na sasa hivi mwanachama anayetaka kugombea jimbo anatakiwa kuandika barua  makao Makuu.

‘’Huu ni utawala wa  ki-ubwenyenye ndani ya chama kuwafanya wapinzani wako wakudhuru   au wakuzidi kete kwa mbinu za kujuana makao Makuu na  Kitendo cha mwenyekiti wa chama Mhe,Freeman Aikael Mbowe (Mb) kiongozi wa kambi Rasmi ya upinzani kuropoka, eti Ndugu Slaa atakuwa ndiye ngombea uraisi  mwaka  2015 ni cha kuua kabisa  Demokrasia ndani ya Chadema’’ 
‘’Tena ninamshauri bure kakangu ninayemheshimu kwa siasa zake; atubu kama aliwahi kumshambulia Yusuf Makamba alipokuwa katibu mkuu – CCM aliposhilia bango, kuwa mgombea mwenye mtaji ni Jakya Kikwete. Mbowe awaombe radhi wanachama na wananchi wapenda mabadiliko. Hawezi kuwaburuza wasomi kama  prof. Baregu, Prof. Safari, Dk. Kitila Mkumbo  na wengine wengi’’ alisema Mwamalala.

Alisema yeye angeulizwa kuwa nani anafaa kuiendesha Chadema ngazi ya Taifa angemtaja Dk. Kitila kuwa awe katiba mkuu wa chama hicho hata kuingizwa kwenye  mchakato wa ugombea nafasi za juu za nchi.

‘’Pia ndani ya Chadema kuna migogoro isiyo na suluhu wa mlingano katika kuitatua, Mfano ni Mwanza na Arusha, chama kimefukuza Madiwani, lakini Karatu nyumbani kwa Dr. Slaa wanabembelezwa, hapa pana ajenda ya kuifanya Chadema iwe ni SACCOS tu huku   maandamano ya kudai haki’’

‘’Hata siku moja hayajaitishwa Moshi, Karatu ili nako wananchi wa kule waonje joto ya jiwe kupambana na polisi, Maandamano ni Mbeya, Mwanza, Arusha ambako viongozi wao wanafukuzwa wakiongea ukweli au kutoa hoja zenye mantiki’’ alisema Mwamalala
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family