
Kuna habari kwamba mchezaji kipenzi wa timu ya Chelsea F.C. ya Uingereza
Frank Lampard huenda akijiunga na timu ya LA Galaxy ya Marekani,
mchezaji mwingine Muingereza, David Beckham ambaye alikua akiichezea
timu hiyo ya California kwa sasa ni muda kama miezi 2 tangia aamue
kutundika daruga.
Frank Lampard aliambia Goal.com amekubali kujiunga na LA Galaxy lakini
msemaji wa LA Galaxy alipoulizwa hakukubali wala kukanusha kwa mchezaji
huyo kujiunga na timu yao.
