JOHN KITIME AUKANDIA UCHUMBA WA JOKATE


SIKU chache baada ya kuwepo kwa madai kuwa model ambaye pia ni Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo amechumbiwa, mwanamuziki mkongwe John Kitime ameingiza utani kwenye jambo hilo kwa kumlaumu kulifanya kuwa la siri kama kweli lipo.


Kupitia blog yake mzee Kitime aliandika hivi: “Mimi na Watanzania wenzangu tumepata mshtuko baada ya kusoma habari hii. Mpaka sasa tunajiuliza ‘why Jokate Why?’ 


“Wewe unaelewa taratibu kuwa mtu anapotaka kuchumbiwa huwa haifanywi siri.


“Jambo la kwanza unaenda kwa afisa utamaduni kuomba kibali ambacho unatakiwa kukipitisha vituo vya polisi vya jirani kisha kibali hicho kupigwa mhuri na katibu mtendaji wa kata unayotegemewa kuchumbiwa na hatimaye kupitia kwangu Afisa Vibali vya Kuchumbiwa, ambapo nitaita Press Conference kutangaza uchumba. Umevunja sheria namba 6 ya 1956 ya Uchumbalization Act...”


SOURCE-TANZANIA DAILY 
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family