| Mzee Small afariki Dunia.
Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi
punde zinaarifu kuwa Mwigizaji maarufu
na mkongwe katika fani ya vichekesho
nchini Tanzania, Said Ngamba maarufu
kwa jina la Mzee Small (59) amefariki
dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mzee Small amefikwa na umauti majira ya
saa 4 za usiku wa Juni 7, 2014 katika
Hospitali ya Taifa Muhumbili.
Akiongea kwa njia ya simu mke wa
marehemu, Bi Fatuma Saidi,
ameithibitishia Father Kidevu Blog, kuwa
Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe
amefikwa na umauti baada ya hali yake
kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na
kumbikiza Muhimbili ambako alishinda
nae akipatiwa matibabu na majira ya saa
tatu usiku alirudi nyumbani na kumwacha
kijana wake akimwangalia mgonjwa na
ilipotimu saa tano usiku kijano huyo
alirudi na kusema baba amefariki.
“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa
ni maneno machache yaliyobenba uchungu
mzito kufuatia kifo cha mumewe.
Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani
kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es
Salaam. |