![]() |
| Tukiwa
na wiki moja toka tumzike muongozaji na muigizaji Adam Kuambiana leo
asubuhi imetoka taarifa nyingine ya kifo cha miongoni mwa waigizaji wa
kike toka Bongo Movie. Aliefariki ni mwigizaji anaitwa Rachel Haule ambaye kacheza movie mbalimbali ikiwemo Vanesa in Dilema. |
![]() |
| Chanzo
cha kifo chake chake bado hakijafahamika ingawa taarifa za mwanzo
zinasema alikua mjamzito na alikwenda Muhimbili kwa ajili ya kujifungua
baadae alifanikiwa kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki
nae hali ilibadilika akapelekwa ICU lakini baadae akafariki. Hii ni status yake ya mwisho Facebook. |
![]() |
| Moja ya waigizaji walioandika kuhusu kifo cha Rachel ni Shilole >>>
‘sitaki kumkufuru Mugu wangu ila kazi yake haina makosa, tulimpenda ila
mwenyenzi Mungu kampenda zaidi, duh.. inauma sana pole Saguda kwa
mtihani uliokupata ila tupo pamoja kwa kipindi hiki kigumu’
|



