Naibu
Waziri
wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen
Massele akifuatilia maelezo toka kwa wajumbe toka Jamhuri ya Czech
walipofika
ili kuanzisha ushirikiano wa kibiashara katika sekta za nishati na
madini kati ya Tanzania na Czech. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje Jamhuri ya Czech Mhe. Tomas Dub na kushoto kwake ni Kamishna
msaidizi wa
madini anayeshughulikia leseni Injinia John Nayopa.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen
Masele akimsikiliza kwa makini Naibu waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Czech
Bw. Tomas Dub alipoongoza ujumbe toka nchi yake ili kuja kuanzisha ushirikiano
baina ya Tanzania na Czech hususan
katika masuala ya uwekezaji sekta za nishati na Madini. Kushoto kwake ni
Kamishna wa Madini anayeshughulikia leseni Injinia John Nayopa.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen
Masele katika picha ya pamoja na ujumbe toka jamhuri ya Czech mara baada ya
kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya
Nishati na madini.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen
Masele akiagana na Naibu waziri wa Mambo ya nje wa Jamhuri ya Czech Bw. Tomas
Dub mara baada ya kumaliza kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake.
Ugunduzi wa
gesi na mafuta wavuta mataifa ya mbali kutafuta fursa za kuwekeza nchini.
Kutokana na ugunduzi wa gesi asilia
na mafuta nchini, Tanzania imeonekana kuwa na thamani kwa nchi mbalimbali duniani
na kuiangalia nchi hii kwa namna tofauti
na ilivyokuwa awali kwani sasa imeonekana kuwa na utajiri mkubwa.
Ugunduzi huu umepelekea Wizara ya
Nishati na Madini kupokea wageni wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika
ili kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya
kibiashara baina ya nchi husika.
Hivi karibuni wizara ya Nishati na Madini imetembelewa na ujumbe toka
Jamuri ya Czech nchi ndogo miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika
kwa lengo la kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha
uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Ujumbe huu uliongonzwa na Bw. Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya
Nchi ya Czech aliyeelezea uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na
madini na kusema kwamba awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa
maji, gesi pamoja na nishati jadidifu,
na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.
Dub alieleza kuwa maendeleo si tu
kutegemea utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia bali inatakiwa nchi ifanye
nguvu ya ziada katika kuongeza thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu
kwa kujenga viwanda jambo lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.
Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka
Wizara kuelimisha watanzania katika chuo
cha madini katika nchi hiyo na kwamba mawasiliano yataendelea kufanyika ili
kufikia malengo ya uhusiano huo.
Kwa upande wake Masele amesema kwamba
zipo fursa nyingi za uwekezaji nchini
katika sekta ya madini na zaidi madini
ya viwandani lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia ugunduzi wa gesi na
mafuta vitalu vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech kuomba vitalu hivyo ili
kuweza kushiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi.
