“Tunawashukuru wauguzi, manesi na madaktari waliomhudimia kwa siku
zote alizokaa hospitalini hapo, wameishi vizuri na majeruhi wetu hadi
leo tunapomsafirisha,” alisema Kamanda Zelothe.
Katika ujambazi huo watu watatu walifariki dunia kwa kupigwa risasi,
wakiwemo askari wawili ambao ni Mkuu wa Upelelezi F. 8106, Nurdun
Kassim Sif (38), DC Robert F. 5339 (33) na raia Hamza Msangaluwa, ambao
walifariki dunia papo hapo.
Ujambazi na mauaji hayo yalifanyika Januari 12, saa 10 jioni kwenye
msitu wa Kijiji cha Kidumi baada ya mtu aliyesadikiwa kuwa jambazi
kufika katika kituo cha Camel akitaka kuuziwa mafuta. |