
Rais wa Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Sheni
(kulia) akimtunuku Dkt.Salim Ahmed Salim nishani ya Mapinduzi ya
Zanzibar jana katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar jana.Picha na Michael
Matemanga
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein
atawaongoza maelfu ya wananchi wa Zanzibar, kusherehekea miaka 50 ya
Mapinduzi ya visiwa hivyo leo.
Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa
pia na Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali
akiwamo Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Ikililou Dhoinine wa Comoro na
maseneta kutoka miji ya Lamu na Mombasa nchini Kenya, pamoja na
mwakilishi maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Vuga mjini Unguja jana, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi
Seif Ali Idd alisema kuwa sherehe hizo ambazo ni kilele zitaanza saa
3.00 asubuhi baada ya viongozi wa kitaifa kuwasili, ambapo pamoja na
mambo mengine Dk Shein atalihutubia taifa hilo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa, wananchi wa
visiwa hivyo wanamtarajia Rais Dk Shein kuzungumzia hali ya kiuchumi,
kisiasa na kudumisha usalama wa raia kutokana na vitendo vya watu
kumwagiwa tindikali, pia harakati za viongozi wa dini na wanasiasa
kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar