
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Philiph Mangula
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM), umeshauri Kamati ya Maadili ya CCM kuwaonyesha mlango wa
kutokea wote walioanza kampeni za kugombea urais, ubunge na nyingine
kinyume cha maadili ya chama.
Umesema wagombea hao ambao umewaita
wasio rasmi, wameonywa mara kadhaa na viongozi wa chama ikiwamo kupitia
kwenye vyombo vya habari, lakini wameshindwa kujitambua na
kujirekebisha.
UVCCM umedai wagombea hao wasio rasmi
katika kampeni zao tayari wameanza kusababisha kutoweka kwa mshikamano
ndani ya chama, kwani wamekuwa wakipita nchi nzima kushawishi kwa fedha
na rushwa nyingine mbalimbali makundi ya jamii ili kuungwa mkono.
Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na
Chipukizi Taifa, Paul Makonda alisema Kamati ya Maadili ya CCM ina
wajibu wa kutafsiri hasira ya wanaCCM dhidi ya kampeni hizo ambazo
zinakijeli chama, uongozi wa nchi uliopo na kuleta nyufa