
Utata umeibuka kuhusu wabunge
waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira kuwa wanahusika na biashara ya pembe za ndovu.Wakati Ofisi ya
Bunge ikidai kuwa ripoti hiyo haina majina ya wabunge, Mwenyekiti wa
kamati hiyo, James Lembeli ameshikilia kuwa majina hayo ni sehemu ya
ripoti hiyo ambayo baada ya kuwasilishwa, iliibua mjadala ambao
ulisababisha mawaziri wanne kuong'oka.
Gazeti hili limedokezwa kuwa majina ya
wabunge hao yalitajwa mbele ya kamati hiyo wakati ikichunguza jinsi
Operesheni Tokomeza Ujangili ilivyotekelezwa, baada ya kuwapo kwa
malalamiko ya vitendo vya ukatili na utesaji wa raia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa
hizo, wabunge hao hawakuitwa mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kutokana na
kwamba suala hilo halikuwa moja ya hadidu za rejea walizopewa
kuzitafutia majawabu.
"Sisi tulimaliza kazi na kuikabidhi
Ofisi ya Bunge, ni kweli majina hayo hayamo kwenye ripoti (iliyosomwa
bungeni) lakini nilikuwa navyo kwenye viambatanisho na ushahidi wake,"
alisema Lembeli jana.
Alipoulizwa sababu za kutokuweka
majina ya wabunge hao katika taarifa iliyosomwa bungeni Desemba 20,
mwaka jana, mbunge huyo wa Kahama alisema: "Hiyo haikuwa kazi yetu sisi
tulikuwa na wajibu wa kueleza yaliyotokana na Operesheni Tokomeza tu,
lakini hayo mengine yapo kwenye viambatanisho
SOURCE MJENGWA
