MAJINA YA WABUNGE MAJANGILI " SIRI KUBWA "

Utata umeibuka kuhusu wabunge waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuwa wanahusika na biashara ya pembe za ndovu.Wakati Ofisi ya Bunge ikidai kuwa ripoti hiyo haina majina ya wabunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli ameshikilia kuwa majina hayo ni sehemu ya ripoti hiyo ambayo baada ya kuwasilishwa, iliibua mjadala ambao ulisababisha mawaziri wanne kuong'oka.
Gazeti hili limedokezwa kuwa majina ya wabunge hao yalitajwa mbele ya kamati hiyo wakati ikichunguza jinsi Operesheni Tokomeza Ujangili ilivyotekelezwa, baada ya kuwapo kwa malalamiko ya vitendo vya ukatili na utesaji wa raia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao hawakuitwa mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kutokana na kwamba suala hilo halikuwa moja ya hadidu za rejea walizopewa kuzitafutia majawabu.
"Sisi tulimaliza kazi na kuikabidhi Ofisi ya Bunge, ni kweli majina hayo hayamo kwenye ripoti (iliyosomwa bungeni) lakini nilikuwa navyo kwenye viambatanisho na ushahidi wake," alisema Lembeli jana.
Alipoulizwa sababu za kutokuweka majina ya wabunge hao katika taarifa iliyosomwa bungeni Desemba 20, mwaka jana, mbunge huyo wa Kahama alisema: "Hiyo haikuwa kazi yetu sisi tulikuwa na wajibu wa kueleza yaliyotokana na Operesheni Tokomeza tu, lakini hayo mengine yapo kwenye viambatanisho
SOURCE MJENGWA