
BINTI anayeshikilia Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike ya Ziff 2013, Elizabeth Michael maarufu Lulu ameweka wazi kuwa amepata mchumba na kwamba taratibu za kujitambulisha na mahari vitafuata baadaye. (HM)
"Unajua mimi ni binadamu na ili
nitulie na kujiepusha na majanga, ni vyema kuwa na mpenzi mmoja
mwaminifu, anayenijali mimi na kazi yangu hapo nitasimama na kusema
kwamba nimepata sehemu ya kutulia na kuanza maisha mapya ya uhusiano na
ndoa," anasema Lulu.
Hata hivyo anasema yeye na mchumba
huyo (ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake) wana mikakati mingi katika
kuyafikia maisha ya uhusiano yaliyo wazi na yenye baraka za wazazi.
"Siwezi kukutajia jina kwa sasa
itafika wakati atajulikana tu, hata hivyo bado hatujafikia hatua muhimu
ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa wazazi na masuala ya mahari na
ndoa. Vitu kama hivi vitafanyika baadaye mwaka huu, hata hivyo wazazi
wangu sidhani kama watakuwa na pingamizi katika hili kwani mimi ni mtoto
wa kike na nimekua sasa," anasema.
Kuhusu Mama Kanumba Lulu anasema: "Huyu ni mama yangu hana tofauti na
mama Lulu hivyo anajua kila kitu na amenipa baraka zake zote, yaliyopita si ndwele kinachotakiwa ni kuganga yajayo, namshukuru mama kwani amenionyesha upendo wa kweli na kunishauri katika maisha, bila yeye nisingekuwa na ujasiri nilionao sasa.
mama Lulu hivyo anajua kila kitu na amenipa baraka zake zote, yaliyopita si ndwele kinachotakiwa ni kuganga yajayo, namshukuru mama kwani amenionyesha upendo wa kweli na kunishauri katika maisha, bila yeye nisingekuwa na ujasiri nilionao sasa.
"Mama Kanumba ni rafiki yangu wa
ukweli, ana mapenzi mazito sana kwangu amekuwa mstari wa mbele
kunishauri na kunipa mwongozo wa maisha ni nini na wapi nilipokosea na
natakiwa kufanya nini ili kuwa na maisha yaliyonyooka," anasema
mwigizaji huyo anayetamba na filamu ya Foolish Age.
Lulu mwenye miaka 19, anasema haikuwa
rahisi kwake kufikiria kutulia kiuhusiano ila amepewa mwongozo bora
unaomfanya afikirie kufanya hivyo kwa sasa.
"Mimi ni binti na kama ujuavyo nina
mapenzi yangu moyoni, si kazi rahisi kuamua kwa sasa lakini nimepewa
mwongozo bora na kuona nini natakiwa kufanya. Kama binti napaswa
kuzingatia maadili, mimi ni kioo cha jamii, inafika hatua inabidi niishi
katika maadili hilo ndilo ninalolifanya sasa."
Anasema wazazi wake wamempa baraka
zote kuhusu uhusiano wake wa sasa: "Wazazi wangu sasa wanafahamu kwamba
nimepata mchumba, kwa kweli wamenipa baraka zao zote, pande zote hata
Mama Kanumba. Nimekua sasa na mimi nina uamuzi wangu, ni vema kuangalia
ninataka nini lakini kikubwa wananishauri."
Anasema wazazi wake hawakubali kila
anachokitaka: "Sina wazazi wa kukubali kila ninachokitaka ila nina
wazazi waelewa, wenye kuangalia jambo kabla hawajaniambia sasa unaweza
kuendelea, mama yangu ni mkali sana, hana mchezo hasa pale anapoona
kwamba nayumba kimaisha," anasema Lulu.
Kuhusu tetesi zilizoenea kwamba ana
uhusiano na msanii wa hip hop Young Dee, Lulu alikana na kusisitiza
kwamba hajawahi hata kuwa na ukaribu na msanii huyo.
"Nashangaa taarifa hizo watu wanazitoa
wapi na mpaka leo nashangazwa na uvumi ulioenea kwamba tulifumaniwa,
usiku ule nilikuwa sehemu nyingine tofauti kabisa, ukweli ni kwamba
sijawahi kuwa na ukaribu na Young Dee, wala hata kumfikiria kama
ninaweza kuwa na uhusiano naye. Bado, hatulingani kwa kweli," anasema
Anayatamani haya
Japokuwa Lulu amepata mchumba, anasema
katika maisha yake alikuwa akitamani kuyapata mambo yafuatayo ili awe
amekamilika kama mwanamke.
"Nina mchumba lakini katika maisha
yangu nilikuwa natamani sana kupata mwanamume mwelewa, atakayenielewa,
atakayeweza kutunza familia na si pesa zitunze familia, nahitaji
mwanamume anayejituma na kujali familia yake.
"Kikubwa zaidi nilikuwa natamani kuwa
na mwanamume atakayeielewa kazi yangu na kila kitu changu. Nashukuru
Mungu kwani yule niliyekuwa namwomba nimempata lakini itategemea siku
zijazo hasa pale kila kitu kitakapokamilika. Nasikitika kwamba siwezi
kumweka wazi kwa sasa, lakini ipo siku nitahitaji watu wamjue," anasema.
Kuhusu msimamo wake kwa mwanamuziki mwenye umri mdogo kutoka nchini Marekani Justine Bieber Lulu anasema;
"Nampenda Justine Bieber japokuwa
nimepata mchumba, mimi ni shabiki wake mkubwa natamani kuolewa naye,
Lulu ni mtu mmoja wa ajabu sana na hafanani na vile watu wanavyomdhania,
ila ipo siku nitahitaji watu wamjue zaidi huyu binti ni nani na ni mtu
wa aina gani," anasema