
Mrembo huyo anadaiwa kumtaka mumewe asaini mkataba mwingine wa miaka mitano wa kubaki Manchester ili kuwasubiri watoto wao; Kai, 4, na Klay mwenye umri wa miezi minane kuwa na umri mkubwa kabla ya kuhama. (HM)
Mkataba ambao Manchester United
inataka kumpa Rooney una thamani ya pauni 65 milioni na utamfanya
straika huyo kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi England.
Kwa sasa analipwa kiwango sawa na
mchezaji mwenzake wa Manchester United, straika wa Kidachi, Robin van
Persie, pauni 250,000 kwa wiki.
Rafiki wa mrembo Coleen, 27, anasema:
"Kitu kikubwa Coleen hataki wahame kutoka Kaskazini Magharibi na jambo
hilo ni muhimu sana kwa Wayne. Hataki kuondoka eneo hilo na kutokana na
kupokea ofa nzuri
ya pesa nyingi anaamini hilo ni jambo muhimu akabaki klabu hapo."
ya pesa nyingi anaamini hilo ni jambo muhimu akabaki klabu hapo."
Manchester United imeipiga marufuku
Chelsea kwamba isithubutu kumfuatilia straika wao huyo kwa sababu
hawawezi kumuuza kwa wapinzani. Real Madrid pia inafukuzia saini ya staa
huyo wa Old Trafford.
Lakini, Coleen hayupo tayari kuona
watoto wake wakihamia London wangali wadogo hivyo, ukiweka kando
Hispania. Anachotaka yeye waendelee kubaki Manchester hadi hapo baadaye.
Familia hiyo inaishi Prestbury,
Cheshire, na wazazi wa Coleen, Colette na Tony wanaishi umbali wa maili
50 huko Formby, Merseyside, karibu na familia ya akina Rooney.
Coleen amesema Rooney, ambaye alijiunga na Manchester United akitokea Everton mwaka 2004,
atapata shida sana kutulia kama atacheza bila ya sapoti ya familia zao.
atapata shida sana kutulia kama atacheza bila ya sapoti ya familia zao.
Lakini, kuna mtazamo tofauti wakati
kocha David Moyes akihaha na kuafiki mshahara wa pauni 300,000 kwa
Rooney, wachambuzi wa soka wanadhani Manchester United inapaswa
kulichukulia kwa hadhari suala la mchezaji huyo.
Staa huyo tayari anaonekana kuiringia
Manchester United kwa kuweka kando suala la kusaini mkataba mpya
akisubiri hatima ya klabu mwishoni mwa msimu kama itakuwa ndani ya nne
bora na kama klabu hiyo itafanya usajili wa mastaa wapya.
Moyes amemnasa Juan Mata kutoka
Chelsea, lakini hilo bado haliwezi kuwa dawa ya kumbakiza Rooney Old
Trafford kutokana na matakwa ya staa huyo kwamba anataka wachezaji
makini waongezwe kikosini.
Kwa sasa kikosi cha Manchester United
kinahitaji mabeki wazuri, viungo wazuri na mshambuliaji mpya mzuri.
Wachezaji hao wakifika huenda timu itafufuka na kuwa tishio zaidi.
Lakini, kitu cha kukumbuka ni kuwa kupata timu kama ya awali ya kushitua
Dunia kutahitaji muda kiasi na umakini mkubwa. Anza na mfano huu;
Januari 3 mwaka huu, straika mahiri wa
Borussia Dortmund, Robert Lewandowski alisafiri kwenda Munich,
Ujerumani na akasaini mkataba wa awali na wapinzani wao wakubwa kwenye
Bundesliga, Bayern Munich.
Bado hajahamia rasmi kwenye timu hiyo
lakini atatua baada ya msimu huu. Suala kwamba Lewandowski angeondoka
akiwa huru haikuwa habari, kila mtu alifahamu hilo.
Kitu pekee kilichokwamisha mpango huo
mpaka sasa ni ukweli kwamba Borussia Dortmund hawakutaka kumuuza, kisa,
walimwona kuwa ni staa wao na walitaka abaki klabuni hapo baada ya Mario
Gotze kwenda Bayern Munich.
Borussia Dortmund iligoma kupoteza
wachezaji wawili kwa mara moja licha ya kutambua ukweli kwamba mapema
tu, Lewandowski alionyesha dhahiri hataki kubaki na timu hiyo.
Kitu hiki kinafanana na suala la
Rooney. Mwishoni mwa msimu uliopita, staa huyo alielezwa kwamba anataka
kuondoka. Jambo hilo bado lipo kwenye akili yake kutokana na sasa
kusuasua kusaini mkataba mpya japo Manchester United wanaamini kwa
kutumia pesa watafanikiwa kumbakiza.
Borussia Dortmund waliamua kumbakiza
Lewandowski katika klabu hiyo mpaka mkataba wake utakapomalizika kabisa,
hawakujali kwamba watampoteza akiwa huru yaani watakula hasara.
Suala la Gotze na Lewandowski,
halikuwa hivi hivi tu, wachezaji hao walifahamu kuwa wakihamia Bayern
Munich watakusanya vikombe na fedha, walifahamu kama wangebaki Borussia
Dortmund wasingepata fedha nyingi. Mashabiki wa Borussia Dortmund
wamekasirika lakini ukweli unabaki pale pale kwamba wachezaji wamefanya
uamuzi ambao wanaamini una manufaa kwao.
Ukimtazama Matthew Le Tissier, yeye
aliamua kuchezea Southampton kwa mapenzi matokeo yake akashindwa kupata
ubingwa wowote. Huenda Le Tissier ni tofauti na Lewandowski, yeye
alipenda klabu yake Southampton na alijiona mwenye furaha, kwa hiyo
akatulia. Leo kuna watu wanafurahia uaminifu wa Le Tissier, lakini
wengine wanamlaumu kwa kukosa mtazamo mpya.
Lewandowski asingefanya jipya
Swali kwa Borussia Dortmund ni je,
walikuwa na sababu za kumfanya Lewandowski abaki kwenye klabu? Kumbakiza
kusingesababisha mabadiliko makubwa klabuni hapo katika ushindani wa
ligi ya ndani.
Bayern Munich watakapokuwa na
Lewandowski watakuwa na faida kwa sababu kwanza straika huyo atataka
kuifanyia kitu klabu yake mpya tofauti na kama angeendelea kubaki
Dortmund.
Kitu hiki kinataka kufanana na Rooney.
Manchester United inaweza kushinda vita ya kumbakiza Rooney Old
Trafford, lakini je mchezaji huyo ataendelea kubaki na moyo wa kuichezea
timu hiyo.
Dortmund kama ingemuuza Lewandowski kwenye majira ya kiangazi mwaka jana ingetengeneza zaidi ya Euro 20 milioni.
Wangetumia pesa hiyo kusaka
mshambuliaji mwingine mzuri zaidi ambaye angewapa faida. Kitu pekee
ambacho Dotmund wanashikilia ni kuwa bado wapo kwenye Ligi ya Mabingwa
Ulaya na kwamba kuwa na mshambuliaji wa aina ya Lewandowski kutawafanya
kuwa tishio.
Anaweza kuwasaidia kwa sasa lakini
ukweli unabaki pale pale kwamba Dortmund wanakubali kuendeshwa na moyo
kuliko akili. Wamesahau kuwa muda unakwenda na watamtoa mchezaji huyo
bure.
Rooney ni kama Lewandowski
Suala la Lewandowski pia lilikuwa
likiangaliwa kwa karibu na Manchester United ambayo ilitaka kumnunua
mchezaji huyo kuchukua nafasi ya Wayne Rooney ambaye alikuwa mbioni
kuondoka. Rooney bado yupo lakini mkataba wake unamalizika mwishoni mwa
msimu ujao yaani Juni 2015.
Mtu anaweza kujiuliza ni kwa kiasi
gani Rooney aliumia wakati timu yake ilipochapwa mabao 3-1 na Chelsea
wikiendi iliyopita. Maumivu yake hayaishii kwenye mchezo huo pekee,
anaumia kwa sababu anafahamu katika siku za karibuni hawatakuwa na uwezo
wa kuwafunga wapinzani wao kirahisi.
Anafahamu wazi kuwa kwa sasa mambo mawili yanatendeka kwa Chelsea, huenda wamefikia
kiwango cha juu au wanakaribia, hivyo kuwashusha itakuwa ni hadithi nyingine.
kiwango cha juu au wanakaribia, hivyo kuwashusha itakuwa ni hadithi nyingine.
Kitu kingine kinachomuumiza ni ukweli
kuwa kwa sasa timu yake inatakiwa kuchongwa upya, na suala hilo linaweza
kuchukua zaidi ya msimu mmoja. Kibaya ni kwamba kengele ya miaka nayo
inagonga, Oktoba mwaka huu anatimiza miaka 29, huenda kwa sasa ana
mawazo kama ya Robin van Persie, alipoona kengele ya miaka yake hapo
2012 akiwa Arsenal, aliamua kutimkia Manchester United kuchukua chake
mapema.
'Chukua chako mapema' ni msamiati
mbaya kwa mashabiki na klabu, lakini msamiati huo una maana kubwa kwa
wachezaji. Rooney alishinda tuzo ya PFA mwaka 2010 akicheza kama
mshambuliaji wa kati na hivi karibuni alisisitiza kuwa hiyo ndio nafasi
anayoipenda zaidi. Kizuri ni kwamba Jose Mourinho anamtaka akacheze
kikosi kwake kama mshambuliaji wa kati akiwa Chelsea na hatakuwa na kazi
kubwa kama anayofanya Manchester United kwa sasa.
Ushawishi wa kocha Moyes
Kocha wa Manchester United, Moyes
amekuwa akijaribu kumtuliza Rooney kwa kumwambia angoje kuvunja rekodi
ya Bobby Charlton ya kuwa mfungaji namba moja wa klabu, lengo likiwa ni
kumbembeleza abaki kwenye klabu. Lakini je, Rooney anajali kuwa mpachika
mabao namba moja wa Old Trafford?
Mabao yake yanaweza kuongezeka hata
akiwa Chelsea, huko atakimbiza rekodi ya Alan Shearer, ambaye alifunga
mabao 260 kwenye Ligi Kuu England.
Anaweza kukimbiza rekodi hiyo akiwa
Chelsea kama mshambuliaji wa kati kuliko kuwa mshambuliaji wa nyuma ya
Van Persie, Manchester United.
Sababu nzuri za kumuuza
Rooney amebakiza miezi 12 tu, kabla ya
kuwa na uhuru wa kusaini mkataba wa awali na Chelsea. Itakuwa ni jambo
la busara kwa Manchester United kumuuza kabla jambo hilo. Hizi ndio
sababu za kumuuza: Kwanza Man United wameshaona kiwango chake mpaka
mwisho, miaka mitano ijayo hawezi kuwa bora kama miaka mitano ya nyuma.
Mbili; Kuna wasiwasi huenda Manchester
United wasishiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakimuuza watapata
fedha za kununua mchezaji mpya, tena chipukizi wenye uwezo wa kuifanya
timu hiyo kuwa bora zaidi.
Tatu: Kumuuza mchezaji nyota si mwisho wa timu bali ni mwanzo wa ustawi. Kwa
mfano, Arsenal kwa sasa ni bora kuliko alipokuwepo Van Persie.
mfano, Arsenal kwa sasa ni bora kuliko alipokuwepo Van Persie.
Liverpool ilimuuza Fernando Torres
kwenda Chelsea watu walilalamika, lakini sasa wameopoa kifaa cha ajabu,
Luis Suarez na Liverpool imekuwa tishio pengine kuliko Torres alipokuwa
na kikosi hicho cha Anfield