
NI balaa. Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na suala hili. Ni hivi mzozo unazidi kutokota miongoni mwa klabu za nchini kuhusiana na stahili wanayodai kuhusiana na uhamisho wa kiungo mkabaji wa Southampton, Victor Mugubi Wanyama, kutinga Ligi Kuu England. (HM)
Klabu kadhaa ambazo zimekuwa
zikitarajia kupata fidia ya kukuza kipaji cha nahodha huyo wa Harambee
Stars, zimesema bado hazijapokea fedha hizo wanazopaswa kupewa ikiwa ni
miezi saba sasa tangu alipotua England akitokea Celtic ya Ligi Kuu
Sctoland.
Uhamisho wa Wanyama wa dau la Sh1.68
bilioni, ulitoa matumaini makubwa kwa timu za nchini alizowahi kuchezea
mwanasoka huyoc kwani zinaamini zinastahili kunufaika kwa mgawo wa
fedha.
Hata hivyo matumaini ya klabu hizo
yanaonekana kugeuka kuwa ndoto baada ya Chama cha Soka England (FA)
kuchelewesha suala hilo kutokana na kuwepo na vuta nikuvute ya timu zipi
ndiyo zina uhalali wa kupata mgawo.
Habari zinasema FA imeamua kusita, kwa kuwa taarifa za Wanyama zimekuwa na utata.
Novemba mwaka jana, FA iliripotiwa
kukataa kupokea pasipoti ya Wanyama iliyowasilishwa mbele yake kwa mara
ya pili kwa maelezo kuwa ilikuwa ikikinzana maelezo na ile ya awali
iliyotumwa na mamlaka za soka nchini.
Nairobi City Stars ni miongoni mwa timu zinazotarajia kunufaika na Sh8 milioni kutokana na dili la Wanyama.
Ili kujihakikishia kupata fedha hizo,
inadaiwa kuwa klabu hiyo kwa msaada wa wanasheria, imemwandikia barua
Wanyama kumtaka asaidie katika kutatua tatizo hilo kwa kueleza kwa kina
ni timu zipi alizozichezea nyumbani kabla ya milango ya neema
kumfungukia na kujikuta Ulaya.
City, miongoni mwa timu
zitakazoshiriki Ligi Kuu Kenya msimu huu, haina wadhamini. Kwa maana
hiyo inazisubiri kwa hamu fedha hizo.
Fedha hizo ni zaidi ya zinazotolewa na Super Sport (Sh5 milioni kwa kila timu ya ligi kuu).
Timu nyinginezo zinazotolea macho
mgawo wa fedha hizo ni pamoja na AFC Leopards, Mathare United na JMJ
Academy. Chanzo: spotikenya