LEMBELI ATAKA WATANZANIA WAAMUE UKWELI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amesema anawaachia Watanzania waamue mkweli kati ya kamati yake na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.Kauli hiyo ya Lembeli inafuatia taarifa ya gazeti moja la kila siku (Siyo Mwananchi), iliyomnukuu Nyalandu akisema ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyowang'oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.
Nyalandu anadaiwa kutoa kauli hiyo alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma na Manyara kuhusu mgogoro wa mipaka kati wanavijiji na Hifadhi ya Tarangire.
Pia, mgogoro huo unahusisha Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani.
Nyalandu alikaririwa akisema kutokana na taarifa hiyo kueleza wapo watu waliobakwa wakati siyo kweli. Tanzania imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora kutokana na ukiukwaji haki za binadamu.
Hata hivyo, Lembeli alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na kauli hiyo alijibu: "Sijaisoma hiyo habari ila nimeisikia tu, kama ni kweli ametoa kauli hiyo (Nyalandu) basi ni hatari."
Lembeli alisema anawaachia Watanzania kupima mkweli kati yake, kamati yake na Waziri Nyalandu katika jambo hilo
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family