ALLY OMARY CHITANDA
MWENYEKITI WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
30/11/2013
KATIBU WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
YAH; KUJIUZURU UENYEKITI WA MKOA
Somo la hapo juu lahusika.
Napenda
kuchukua nafasi hii kukuarifu kuwa kwa hiari yangu bila ya kushawishiwa
na mtu yeyote, nimeamua kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa tangu leo
tarehe 30/11/2013.
Nashukuru
sana kwa ushirikiano wako pamoja na Vionmgozi wote wa Baraza la Uongozi
pamoja na Baraza la Mashauriano la Mkoa, lakini pia niwashukuru
Viongozi wote wa Majimbo naWilaya hasa Nachingwea ambao kwa kiasi
kikubwa, wameniwezesha kufika hapa hasa wakati mgumu wa Ujenzi wa
Chama na kugombea Ubunge 2005 na 2010.Matarajio yangu ya kuweza
kukomboa wanyonge kupitia CHADEMA kwa sasa sioni kama yanaweza
kufikika.
Nitabaki
kuwa Mwanachama wa kawaida na ninaahidi kuwa Mwanachama mwaminifu na
pale nitakapohitajika nikotayari kusaidiana na Viongozi kujenga
Chama.Nawataki kazi njema na Ujenzi wa Chama.
Ahsante kwa ushirikiano.
………………………………..
A.O. CHITANDA
========== ======== ==========
MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI, MJUMBE BARAZA KUU TAIFA NA MKUTANO MKUU. KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU WA CHAMA MAKAO MAKAUU
NDG: WANA HABARI:
Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.
Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA,nimejiunga CHADEMA mwaka 2003 nikitokea NCCR –MAGEUZI.
Nyadhifa nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:-
Kuanzia
mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa nikiwakilisha vijana Bara
niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia
Chama, nimewahi kuwa Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na
Haki za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la
Vijana Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha
Nachingwea, Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu tarehe 26/05/2013.Pia ni Afisa Mwandamizi Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.
vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Hivyo
sasa, pamoja na mambo mengine yapo masuala nyeti na muhimu
ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali
pindi itakaponihitaji kufanya hivyo.
Ndugu
zangu wanahabari, nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania
wenzaqngu juu ya hali ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu.
Itakumbukwa kuwa tarehe 20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja
na mambo mengine ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya
Chama alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:-
(a) Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.
(b) Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa endapo angekubali kugombea.
(c) Mhe. Zitto alishindwa
kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa kutoshiriki pamoja na
Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa yaliyokikumba Chama kama:-
(i) Maandamano ya Arusha.
(ii) Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.
MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
Ni
kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia
pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika
utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa
Wakurugenzi watano ambao ni:-
1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Uteuzi
huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo
kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.
Lakini
pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo
sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro
Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.
Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa.
Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini,
hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa
hali na mali.
Mimi kama
nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa niko kwa kwa miaka 10 sasa na
nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika Ujenzi wa Chama hiki.Sioni sababu
ya kutoharakisha kulipa posho ya Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na
watendaji wengine na badala yake tunaharakisha kujilipa posho nono sisi
watendaji wa Makao Makuu, wakati hawa wa ngazi za chini wanamaeneo
makubwa ya Kiutendaji na wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa
kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea wenyewe.
MAAMUZI YA KAMATI KUU.
Ningependa
kuwaambia wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya kamati
kuu ya kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi ya kijuha na
yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu
wapo makini na huo ukombozi wanaousema.
Tumekuwa
tukiweka mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano,
kabla hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati tu
ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa
jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.
Nikiwa
mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na
dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini
hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha
leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi
kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena.
Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.
Naomba
nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara
kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo
thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za
chama kuwajenga wajumbe ndio.
Kwa mfano
hivi sasa tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema mjadala
wa zitto kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama
kuzunguza nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii
si sawa hata kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha
watu binafsi kutimiza matakwa yao ya kisiasa.
Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya watanzania wenzangu. Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu.
Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu. Nafsi
yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa
Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.
Kwa kuwa
siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila mkumbo ni
kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni
kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.
Hivyo
basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua
kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama.
Sioni
tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya kuwa
mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa KATIBU WA
SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Kwa kuwa
vipaumbele vya chadema ni kukijenga chama mikoa ya kaskazini. Basi sisi
wananchi wa mkoa wa lindi tunawatakia kila la heri, na kwamba waendelee
kukijenga chama chao huko huko waliko.
Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu yangu.
Ahsante Sana
A.O. CHITANDA
0753418510
MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI
SOURCE:MICHUZI JR