| Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini
wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile
wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa
Malakal.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi
la Sudan Kusini.
Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu
wengi kupindukia. Watu hao walikuwa
wanatoroka vita vinavyotokota katika mji wa
Malakal.
Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi
Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir
kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais
Riek Machar, kwa kuwa na njama ya
kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya
watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza
nchini humo. |