RAIS KIKWETE AWAAPISHA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MALYSIA NA KAMISHNA WA TUME YA USULUHISHI,IKULU JIJINI DAR

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima 
Picha na Freddy Maro wa Ikulu.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt.Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam.