| Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi. |
Baadhi ya Waendesha Boda Boda wakiwa wamekusanyika sehemu ya mazishi ya kijana huyo.
Mchungaji
Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia
Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha
pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki
aitwaye Gabriel Osward Ngalele.
Vurugu
hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa
ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na
abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu
za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa
hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo
walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa
kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
Hata
hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana
utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi
watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea
mtafaruku mkubwa.
Katika
mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye
makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi
kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake
kwa ulinzi mkali.
Wakati
mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu
za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji
Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha
Ibada ya mazishi.
Katika
mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi
wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye
aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.
Kwa
upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema
amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa
wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na
si waumini wa Kanisa lake.
Aidha
Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua
zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu
na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia. Pia
amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu
wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.
Wakikabidhi
rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma
amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala
ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.
Habari kwa hisani ya Ezekia Kamanga
wa Mbeya yetu