Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.(MM)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni
katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na
Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu
alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba
funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala
nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili
yamasomo.
"Nyaraka zake zinaonyesha marehemu
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla
hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea
mara kwa mara," alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa
funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa
amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa
taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na
kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi
wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha
mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa
marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu
siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza
vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
"Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza
mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika
MachavaHostel ndiko anakolala," alisema Alphonce.
CHANZO: NIPASHE